Mshauri wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Crescentius Magori, amekanusha taarifa za klabu hiyo kuwa na mpango wa kumtoa kwa mkopo Mshambuliaji kutoka nchini Rwanda Meddie Kagere.

Magori ambaye pia anahusika na usajili wa wachezaji klabuni hapo amesema taarifa za Simba SC kuwa tayari kumtoa kwa mkopo Mshambuliaji huyo sio za kweli, na waameshangazwa kuona zinavyoendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Amesema hawana mazungumzo yoyote na APR ya Rwanda inayotajwa kumuwania Mshambuliaji huyo kwa mkopo, na badala yake ataendelea kuwa kwenye kikosi chao kwa msimu ujao wa 2021/22.

“Tunashangaa kuona hizi taarifa kuhusu Kagere, hakuna ukweli wa jambo hilo, Kagere ataendelea kuwa kwenye kikosi chetu kwa msimu ujao.” amesema Magori

Katika hatua nyingine Magori amezungumzia suala la usajili wa kiungo Mshambuliaji Yusuph Mhilu ambaye alizua tafrani kati ya Simba SC na Kagera Sugar kufuatia uahamisho wake kuwa na utata.

Amesema wamefikia hatua nzuri ya kumalizana Kagera Sugar, na wana matumaini makubwa kabla ya kuanza kwa msimu ujao suala hilo litakua limekamilika.

GMS: Msiihukumu Young Africans kwa mchezo mmoja
Rais wa Marekani kulihutubia taifa