Mshauri wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzj Simba SC, Crescentius Magori ameibeza klabu ya Young Africans kwa kusema kikosi chao kilicheza na Vibonde Siku ya Mwananchi.
Magori amesema amesema Zanaco FC iliyoifunga Young Africans siku ya Jumapili (Agosti 29) ni timu ya kawaida sana.
Amesema Young Africans haikupaswa kupoteza mchezo kwa kufungwa 2-1 na Zanaco FC ambayo haipo kwenye orodha ya vilabu 10 bora Afrika.
Maagori amewataka wadau wa Soka nchini kujiandaa kuona burudani safi katika Tamasha la SIMBA DAY itakapofika Septemba 19, Uwanja wa Mkapa.
“Jumapili nimeangia mpira mpaka nimesinzia, Wanacheza mpira gani ule wanacheza kama wanatembea Pressing yao ni ndogo sana.”
“Tarehe 19 ndiyo mtaona mpira sasa, yaani utapigwa mwingi watu wataangikana aaaaaaah.”
“Wamecheza na Zanaco ambayo haipo hata kwenye list ya vilabu 10 bora Afrika na wakapigiwa mpira mwingi vile, waje tarehe 19 wamuone Rally Bwalya, Pape Sakho na mafundi wengine ndo wajue Mpira unavyochezwa.”
Hata hivyo Simba SC bado hawajatangaza timu itakayocheza dhidi ya kikosi chao katika Tamasha la Simba Day, Septemba 19.