Ofisa wa programu wa kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti na mtaalamu wa Tehama, Theodory Giyani wameieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wameshindwa kufikia muhafaka wa makubaliano na mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP).

Agosti mwaka huu washtakiwa hao wamemuandikia barua DPP wakiomba kukiri mashtaka yao ili kuimaliza kesi hiyo.

washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kutakatisha fedha Sh 17 milioni.

kupitia wakili wao Jeremiah Mtobesya wameeleza hayo jana Novemba 10 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega, amesema kuwa wateja wake waliandika barua ya kukiri na kuomba msamaha kwa DPP lakini imeshindikana.

“Tuliandika barua kwenda kwa DPP kwa ajili ya mazungumzo ya kumaliza kesi lakini taarifa zisizo rasmi ni kwamba mchakato huo umeshindikana” alidai Mtobesya.

Awali wakili wa serikali, Ester Martin alidai upelelezi haujakamilika. kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 24.

Taifa Stars yaondoka Uturuki
ACT-Wazalendo yatafakari kujiunga na serikali ya Umoja wa kitaifa