Rais John Magufuli ameahirisha shamrashamra za kikukuu ya kumbukumbu ya siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambazo hufanyika kila mwaka, Aprili 26.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kurungenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, Rais Magufuli amewataka wananchi kusherehekea siku hiyo kwa kupumzika majumbani kwao na katika shughuli zao binafsi.

Aidha, fedha zilizokuwa zimepangwa kwa ajili ya kugharamia vyakula, vinywaji, gwaride na mengineyo ameagiza zielekezwe katika upanuzi wa barabara ya Mwanza ‘Mwanza – Airport’, katika eneo linaloanzia Ghana Quarter hadi katika uwanja wa ndege jijini humo, kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari.

Desemba 9 mwaka jana, Rais Magufuli alitangaza kuahirisha shamrashamra za maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika na kuagiza itumike kwa ajili ya usafi huku mabilioni yaliyotengwa yalielekezwa katika upanuzi wa barabara ya Mwenge – Moroco jijini Dar es Salaam.

Mapenzi: Sehemu 4 za mwili usizopaswa kumshika mkeo nyakati hizi 18+
Stewart Hall Alalamikia Hujuma Ligi Kuu