Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli ameendelea kutangaza kiama cha viongozi wanaoshiriki vitendo vya rushwa na ubadhirifu wa fedha za chama hicho.

Akihutubia wanachi wa Jiji la Mwanza jana katika viwanja vya Furahisha, Rais Magufuli amesema kuwa katika uongozi wake atahakikisha anarudisha hadhi ya chama hicho katika maadili kama ilivyokuwa wakati wa utawala wa Mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho, Mwalimu Julius Nyerere.

Rais Magufuli alisema kuwa atahakikisha ufisadi ndani ya chama hicho unakomeshwa na kwamba mtu yoyote atakayeomba kugombea nafasi yoyote ndani ya chama na akabainika alitumia rushwa kushawishi wananchi ‘atakatwa’.

“Lazima ifike mahala turudishe hadi ya chama kama ilivyokuwa enzi za Mwalimu Nyerere na sio kuwaachia watu wachache wagawane fedha za wananchi,” alisema Rais Magufuli.

“Hivi fedha za majengo ya wanachama mgeweza kugawana walau mara mojamoja. Bahati nzuri nimekuwa mwenyekiti, sasa ni lazima wanachama muanze kuhoji kwenye vikao vyenu haya mapato na wakiwauliza nani anawapa jeuri ya kuhoji waambieni ni Mwenyekiti,” alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ambaye anaendelea na ziara yake mkoani humo, alitoa mfano wa jengo la ghorofa sita linalomilikiwa na CCM ndani ya mkoa huo akieleza kuwa gharama za upangishwaji zimekuwa kizungumkuti kwani huelezwa kuwa ni shilingi 50,000 lakini wakati mwingine gharama halisi huwa ni shilingi 300,000 au 500,000.

Kubenea afunguka baada ya Serikali kulifungia gazeti la Mseto
Shule Za Feza Nchini Kutofungwa