Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ampongeza mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz kwa  kuanzisha kiwanda mkoani Morogoro. 

Aidha Rais Magufuli, amemshukia  mbunge wa Morogoro Mjini  Aziz Aboud kwa kushindwa  kuendesha viwanda viwili alivyokuwa anavimiliki ambapo amesema kuwa ameshindwa kuendeleza viwanda viwili vikubwa cha Calvan na Moplo.

 “Kiwanda cha Moplo kilikuwa kinahusika na mafuta ya kupikia, mimi nasema hadharani sikufichi, ulipewa viwanda tangu  mwaka 1996 hadi mwaka jana walipokunyang’anya uliwanyima ajira hata wapigakura wako,” amesema Magufuli.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo, Ijumaa Februari 12, 2021 wakati wa uzinduzi wa kiwanda  cha Ngozi cha ACE Leather Tanzania Limited-Kihonda, kinachomilikiwa na Rostam.

 Katika maelezo yake Rais Magufuli amesema, “huu ndiyo ukweli na mimi nitabaki siku zote kusema ukweli, nasema uongo ndugu zangu? Abood amekaa na viwanda vya Moplo na Calvan kwa zaidi ya miaka 25.

“Huyu leo simpongezi ingawa jana nilimpongeza kwenye viwanda ndugu Abood hujafanya vizuri. Nikiondoka Morogoro sijasema hili nitakuwa mnafiki,” amesema Rais Magufuli.

 Katika hafla hiyo Rais Magufuli amesema  Kiwanda cha Calvan kiliuzwa kwa  Benki ya CRDB, ambayo hata hivyo hawakukiendeleza, huku akimuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara, Geoffrey Mwambe kusimamia suala hilo na kiwanda hicho kifanye kazi.

Tanzania haijawahi kusema hakuna corona
K light aachia ngoma mpya, Mr Blue, Country boy ndani