Fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha shamrashamra za maadhimisho ya siku ya Uhuru, Disemba 9 zimepangwa kujenga barabara kutoka Morocco hadi Mwenge jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, rais John Magufuli ameagiza kiasi cha shilingi bilioni 4 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hizo kutumika kufanya upanuzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 4.3.

Rais Magufuli amemuagiza Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanrods, Mhandisi Patrick Mfugale kuhakikisha utekelezaji wa kazi hiyo unaanza mara moja ambapo barabara mbili zitaongezwa hivyo kuifanya njia hiyo kuwa na barabara tano.

“Tayari fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni nne zimshapelekwa Tanroads kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo linalopaswa kuanza mara moja,” taarifa hiyo ilieleza.

Miss Tanzania Akumbwa Na Kashfa Ya Ufisadi Wa Shilingi Trilioni 1.3
Posho Za Wabunge Zapigwa Chini