Mgombea urais kupitia CCM, Dk John Magufuli jana alipata mapokezi ya kishindo mjini Kigoma alikofanya mkutano mkubwa na wa kihistoria.

Dk Magufuli alipokewa na umati mkubwa wa wananchi waliofurika katika uwanja wa Kawawa kwa ajili ya kumsikiliza.

Akiwahutubia maelfu ya wananchi hao, Dk Magufuli aliwaomba wananchi hao kumchagua kuwa rais kwa kuwa atachagua mawaziri watakaowatumikia wananchi kwa nguvu zao zote na wataongozwa na waziri mkuu makini.

“Nitateua mawaziri ambao wataweza kwenda na kasi ya maendeleo mtakayohitaji, nitasimamia mimi mwenyewe pamoja na waziri mkuu makini na watakuwa tayari hata kuumwa na mbu, kunguni wakati wote ili mradi wawatumikie watanzania hata usiku wa manane,” alisema.

Magufuli pia aliahidi kuwa serikali yake itawajali walemavu, wasanii pamoja na wanamichezo ili kuongeza kasi ya maendeleo yenye tija kwa taifa.

 

Luke Shaw Afanyiwa Upasuaji
Arsenal Wafuata Madudu Ya Man City, Man Utd