Mikakati ya kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu zimekuwa na utofautia mkubwa ambapo upande wa CCM umeonesha kuzitumia njia za wapinzani kuwavuta wapiga kura.

Ingawa CCM imekuwa na kauli mbiu nyingi za ushawishi, mgombea urais kupitia chama hicho amejivika kauli mbiu maarufu ya kampeni za Chadema ya M4C (Movement for Change) na kudai kuwa kauli mbiu hiyo inamzungumzia yeye kwa ajili ya mabadiliko.

“Wanasema M4C mnajua maana yake? Maana yake ni Magufuli for change,” alisema Magufuli katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika jana Kigoma mjini.

M4C

Magufuli alitumia kauli mbiu hiyo na kuwakejeli wapinzani kwa kutumia picha za wagombea urais wa Chadema, Edward Lowassa anayoonekana akiwa amevaa suti. Aliwaambia wananchi kuwa mgombea huyo hawezi kurudi kwa wananchi kwa kwa mtazamo wa vazi alilovaa.

“Mkiangali hizi picha za wagombewa, mimi nimevaa shati, wmingine amevaa sut, sasa huyu mwenye suti anaweza kukubali kuja kupata shidna na ninyi,” aliwahoji wananchi hao.

Hivi karibuni, Magufuli amekuwa akitumia pia kauli mbiu ya ‘Mabadiliko’ inayotumiwa na Ukawa kuiongoza kampeni yake.

 

UEFA Kuanzisha Changamoto Mpya Kwa Vilabu
Graham Poll Amchana Live Muamuzi Wa Kitaliano