Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli ameshauri daraja la Kigamboni lipewe jina la muasisi wa Taifa hili, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Daraja

Akiongea wakati wa kuzindua daraja hilo leo, Rais Magufuli amesema kuwa awali aliletewa mapendekezo wakimtaka aridhie daraja hilo lipewe jina lake, lakini kwakuwa wazo la ujenzi huo lilianza tangu wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere, alishauri jina hilo litumike.

“Nilikataa hili daraja la Kigamboni kuitwa jina langu kwanza jina langu lenyewe siyo zuri eti Magufuli yaani halileti hata raha. Ila mimi nafikiri kama Wizara ya ujenzi wataona kuna umuhimu, kuna viongozi waliotangulia waliweza kutuunganisha kwa dini zetu, waliunganisha makabila yote na kujenga umoja wetu. Kwenye daraja hili watu wa CCM watapita hapa, watu wa Ukawa watapita hapa, mimi napendekeza hili daraja liitwe daraja la Nyerere,” alisema Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amewataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanalitunza daraja hilo katika kujenga uchumi wa taifa.

ATOLEWA KWENYE NDEGE KWA KUONGEA KIARABU
Mtanzania awa muafrika pekee kubeba tuzo hii kubwa zaidi duniani