Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, ametuma salamu za pole kwa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Pili wa nchi hiyo Daniel Arap Moi aliyeaga dunia usiku wa kuamkia leo.

Rais Magufuli amesema Tanzania itamkumbuka kwa uongozi wake mahiri, jitihada za kuimarisha uhusiano baina ya Kenya na Tanzania pamoja na jitihada zake za kufufua Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Kwa niaba ya Serikali na Watanzania nakupa pole Mhe.Rais Uhuru Kenyatta na Wakenya wote kwa kuondokewa na Rais Mstaafu Daniel Toroitich arap Moi. Watanzania tutamkumbuka kwa uongozi wake mahiri, jitihada za kuimarisha uhusiano wetu na Kenya na kufufua Jumuiya ya Afrika Mashariki” Amesema Magufuli

Taarifa za kifo hicho zimetangazwa alfajiri ya leo na Rais Uhuru Kenyatta, ambapo Moi amekuwa akiugua kwa muda na mara kwa mara amekuwa hospitalini, licha ya kuwa mwenye afya nzuri baada ya kipindi chake cha Urais.

Mzee Moi amefariki leo Februari 04, 2020 alfajiri saa 11 na dakika 20 (5:20am) akiwa na umri wa miaka 95 (ingawa aliyekuwa katibu wake, Lee Njiru amesema marehemu alikuwa na miaka 103).

Jina la mkongwe Giorgio Chiellini latua UEFA
Kenyatta awalilia wanafunzi waliokufa kwa kukanyagana baada ya kengele ya kwenda makwao