Rais Dkt Joh Pombe Magufuli kwa mara ya kwanza ameongelea juu ya ushindi wa Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu, ambalo lilikuwa linashikiliwa na Tundu Lissu, kwa kutoa pongezi.

Akizungumza leo, wakati wa uzinduzi wa rada mbili za kuongozea ndege, amesema kuwa jimbo hilo lilikuwa halina muwakilishi, amefurahi kuona limepata muwakilishi.

” Nimefurahi kumuona Mbunge wa CUF, lakini nimefurahi kumuona Mbunge ambaye jimbo lilitelekezwa  lilikokuwa la Tundu Lissu, saa nyingine majimbo yanakosa uwakilishi” amesema Rais Magufuli na kuongeza kuwa atahakikisha kero ya maji inashughulikiwa katika jimbo hilo

“Sikuile ulitoa maagizo spika tushughulikie tatizo la maji kule, nakuahidi tutashughulikia maji katika jimbo lile, ili yale yaliyochelewa yakamilike kwa haraka haraka” alisema Magufuli.

Mbunge Mtaturu alikuwepo kwenye hafla ya uzinduzi huo wa rada kwani pia yupo kwenye kamati ya miundombinu ya Bunge.

Mbunge Mtaturu yupo kwenye kamati ya miundimbinu ya Bunge na alikuwepo kwenye hafla ya uzinduzi wa rada ambapo Serikali inatekeleza mradi wa ujenzi wa rada nne kati ya hizo, mbili zimekamilika ambazo ni ya Dar es salaam na ya Kilimanjaro.

Ujenzi huo unaendelea katika mikoa ya Songe na Mwanza, jumla ya mradi huo umeghalimu kiasi cha shilingi bilioni 67.3. na sasa Tanzania amekuwa na uwezo wa kuongoza ndege kwa asilimia 75 ya anga.

 

Rais Magufuli: aliyeshikilia ndege Afrika Kusini 'ni wivu tu'
Ndayiragije atangaza watakaoivaa Sudan