Rais John Magufuli amemuapisha Katibu Mkuu Kiongozi Mpya, Balozi John William Kijazi akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Ombeni Sefue.

Kiapo

Mhandisi Kijazi ameapishwa muda mfupi uliopita Ikulu jijini Dar es Salaam, tukio lililoshuhudiwa na viongozi wa wa ngazi za Juu wa Serikali akiwemo Makamo wa Rais, Bi. Samia Hassan Suluhu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Balozi Sefue pia alihudhuria na kushuhuidia kiapo hicho.

Kiapo, 3

Jana, Rais Magufuli alimuondoa Balozi Ombeni Sefue katika nafasi hiyo akieleza kuwa atampangia kazi nyingine baada ya kumteua mhandisi Kijazi ambaye alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India.

Kocha Wa Coastal Union Ampongeza Muamuzi Kwa Kupoteza Point Tatu Ugenini
Messi Na Ronaldo Wamtoa Roho Shabiki Wa Soka India