Dk John Magufuli, mgombea urais kwa tiketi ya CCM ambaye hivi karibubi tafiti za Twaweza na IPSOS zimempa ushindi amewataka wananchi kutozitegemea ripoti hizo na badala yake wajitokeze kumpigia kura Oktoba 25.

Akiongea katika mkutano mkubwa wa kampeni mjini Kahama, Dk Magufuli amewataka wananchi kutojikita katika kuziamini tafiti hizo na kuamini kuwa tayari ameshashinda kwa kuwa bila kumpigia kura ndoto hiyo haitawezekana.

“CCM tusidekezwe na utafiti, nataka kushinda kwa asilimia 95, nendeni mkanipigie kura, manaake wanaweza wakaja watu hapa wakawaambia tumeshinda kwa utafiti. Hapana, siwezi kushinda kwa maneno, nendeni mkanipigie kura Oktoba 25 asubuhi,” alisema Magufuli.

Dk. Magufuli alipokewa na umati mkubwa wa wananchi wa Kahama, jimbo ambalo mbunge anaemaliza muda wake, James Lembeli aliihama CCM na sasa anagombea kwa tiketi ya Chadema.

 

Simba Yanga ni ‘Afe Punda Mzigo Uende’
Lowassa Awaelekeza Wananchi Jinsi Ya Kuwajibu 'Wanaomtukana'