Kampeni za uchaguzi mkuu zimeendelea kuongeza kasi huku kila chama kilichosimamisha mgombea kikitumia kila mbinu kuhakikisha kinawavuta wapiga kura wengi zaidi kwao.

Mbinu ya mgombea urais kupitia CCM, Dk John Magufuli kuibadili na kutumia kauli mbiu ya Chadema ya Movement 4 Change kuwa Magufuli for Change imeendelea kupingwa na upande kambi ya Ukawa.

Sumaye Peoples

Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, jana alimkosoa Dk Magufuli kwa kutumia kauli mbiu hiyo na kudai kuwa kama amenogewa na sera za kambi hiyo ya upinzani anakaribishwa katika umoja huo na kwamba amkabidhi kadi ya CCM mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.

“Tunamshauri kama anaona ndiyo nzuri arudishe kadi ya CCM kwa Lowassa, tunamkaribisha,” Sumaye aliwaambia maelfu ya wakazi wa Mtwara walihudhuria mkutano wa kampeni.

Dk Magufuli ameendelea kusisitiza katika mikutano yake ya kampeni kuwa yeye ndiye alama ya mabadiliko na kwamba M4C inamaanisha ‘Magufuli Kwa Mabadiliko’.

Hivi karibuni, Chadema walieleza kuwa watafungua shtaka dhidi ya mgombea huyo kwa kuiba na kutumia nembo ya chama hicho ambayo wamedai ilisajiliwa kwa kufuata taratibu na sheria za vyama vya siasa pamoja na haki miliki.

Shetta Afunguka Kuhusu Tuhuma Za Kuuza Dawa Za Kulevya
Sir Alex Ferguson: Moyes Alikuwa Sahihi Kwa Man Utd