Mgombea wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli amerusha jiwe gizani kwa mmoja wa wagombea kutokea Singida ambaye hakumtaja jina akiwa katika mkutano wake wa kampeni Ikungi, mkoani Singida leo Septemba 1,2020.
“Mmoja wa Wagombea nafikiri anatoka hapa (Singida) mshaurini kwamba mimi mnipe kura nyingi nitamtafutia kikazi kidogokidogo Serikalini, ni Mtoto wetu tunampenda, mimi sina tatizo na mtu yeyote, kwani kazi lazima uwe Rais?, akija mwambieni kwamba Magufuli amesema atakupa kazi” amesema Magufuli.
“Mgombea anayetoka hapa ni Mtoto wetu tunampenda, mimi sina tatizo na Mtu, Urais muachie Magufuli wewe tutakupa kikazi utakachoweza kufanyafanya, sisi wote ni wamoja, akija mwambieni Magufuli amesema atakupa kazi, kwanini unahangaikia hii kazi ambayo hautashinda!?” ameongeza Magufuli.