Rais John Magufuli ametaja baraza lake la Mawaziri leo huku akilipunguza baraza hilo na kuwa na wizara 18 pekee  kama alivyoahidi wakati wa kampeni zake kuwa ataunda baraza dogo ili kupunguza matumizi ya serikali.

Katika baraza hilo, rais Magufuli ametaja watu 30 watakaounda baraza hilo litakalokuwa na jumla ya watu 34 pekee huku akiziweka kiporo wizara nne. Rais alisema kuwa atateua majina ya mawaziri hao wanne baadae kwa kuwa bado hajawapata.

Baraza la Mawaziri

Katika baraza hilo, rais Magufuli amewarudisha jumla ya mawaziri na manaibu waziri 11 wa Serikali ya awamu ya nne huku baadhi ya wizara zikiwa hazina manaibu waziri.

Hii ndio orodha ya mawaziri katika wizara mbalimbali:

Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora – Simbachawene na Angela Kairuki”

Wizara ya ofisi ya Rais, Utumishi na utawala bora ina mawaziri wawili ambao ni Mh. Simbachawene na Kairuki

Ofisi ya waziri Mkuu,Sera,Bunge,Kazi,vijana,ajira na walemavu,Waziri Jenista Mhagama,Naibu waziri Dk.Possy Abdallah.

Wizara ya Mambo ya Nje na EAC/ Kimataifa – Augustino Mahiga, Naibu Waziri – Dk. Suzan Kolimba

Wizara ya Ardhi – William Lukuvi

Wizara ya Elimu Waziri bado hajapatikana, Naibu Stella Manyanya

Waziri wa Afya jinsia na watoto: Ummy Mwalimu, Naibu wake Ni Dk. Hamisi Kigwangalla

Wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi. Waziri: Mwigulu Nchemba Naibu Waziri: William Tate Ole Nashon

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Waziri wake bado hajapatikana, Naibu Waziri wake ni Edwin Ngonyani

Waziri wa Utamaduni,  michezo na Wasanii: Nape Nnauye

Waziri wa Fedha na Mipango Waziri bado hajapatikana, Naibu Waziri wake ni Dk. Ashantu Kijachi.

Ofisi ya Makamu wa Rais/Muungano na Mazingira,Waziri January Makamba,Naibu waziri Luhaga Mpina.

Wizara ya Nishati na Madini Waziri ni Sospeter Muhongo na Naibu Waziri wake ni Medard Kalemani.

Wizara ya Katiba na Sheria; Waziri ni Harrison Mwakyembe

Wizara ya Mambo ya Nje,Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, Waziri ni Augustine Mahiga N/Waziri Susan Kolimba

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Waziri ni Husein Mwinyi

Wizara ya Mambo ya Ndani, Waziri ni Charles Kitwanga.

 

 

Issoufou Garba Wa Yanga Atua Dar es salaam Kimyakimya
Lowassa Aizungumzia Tena Ikulu