Kazi inayofanywa na Rais John Magufuli imeelezwa kuwa itakuwa sababu ya kuviuwa vyama vya upinzani nchini katika awamu yake.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye aliyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akikagua maandalizi ya sherehe za miaka 39 ya CCM, yanayotarajiwa kufanyika Februari 6 badala ya Februari 5.

Hata hivyo, Nape alieleza kuwa asingependa kuona vyama vya upinzani vinakufa kwa kuwa vinasaidia katika kuleta demokrasia nchini.

Katika hatua nyingine, Nape alieleza kuwa maadhimisho ya mwaka huu ya chama hicho yatakuwa ya kipekee kwani yatafanyika kwa kuwashirikisha wananchi kufanya kazi za maendeleo na kwamba kauli mbiu yao itakuwa ‘sasa kazi’.

Nkurunzinza 'awatupa' nje ya Burundi wanajeshi wa Umoja wa Afrika
Zitto Awarushia Kombora Ukawa kuhusu Kilio cha Uteuzi Kamati za Bunge