Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Desemba 5, 2020 amefanya uteuzi wa Mawaziri 21 na Manaibu Waziri 23.

Akitangaza uteuzi huo ameeleza kuwa Rais Magufuli ameteua Mawaziri 21 na kufanya jumla ya Mawaziri sasa kuwa 23 ikiwa ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango ambao waliteuliwa Novemba 13 mwaka huu.

Katika orodha iliyotangazwa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, baadhi ya mawaziri wamerejea katika nafasi zao, wengine wakipanda kutoka manaibu waziri na kuwa mawaziri kamili.

Mawaziri waliosalia katika nafasi zao ni Profesa Joyce Ndalichako (Elimu), Dotto Biteko (Madini), Jenista Mhagama (Ofisi ya Waziri Mkuu), Selemani Jaffo (TAMISEMI), George Simbachawene (Mambo ya Ndani), Mwigulu Nchemba (Katiba), William Lukuvi (Ardhi), na George Mkuchika (Utumishi).

Baadhi ya Mawaziri wa awamu iliyopita ambao wamerejea lakini wamehamishwa wizarani Ummy Mwalimu ambaye sasa ni Waziri wa Muungano na Mazingira kutoka Wizara ya Afya na Innocent Bashungwa ambaye sasa ameteuliwa kuongoza wizara ya Habari na Michezo akitoka Wizara ya Viwanda.

Waliokuwa Manaibu Mawaziri na sasa wamepanda na kuwa Mawaziri kamili ni Dkt Damas Ndumbaro (Maliasili na Utalii), Dkt Faustine Ndungulile anayesimamia Wizara mpya ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Juma Aweso (Maji).

Balozi Kijazi ameeleza kuwa wateuliwa wote watateuliwa wiki ijayo na muda wa kuapishwa utatangawa.

Hili hapa Baraza Jipya la Mawaziri, Manaibu wao
Serikali kununua ndege zingine 4