Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli ameeleza kile kinachompa nguvu zaidi ya kupambana na wakwepa kodi na mafisadi bila kujali jina au sura ya mtenda kosa.

Akiongea katika mkutano wake na wafanyabiashara mbalimbali na wadau wa sekta binafsi nchini uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, rais Magufuli alisema kuwa wakati wa kampeni zake hakupokea hata shilingi moja ya mchango wa mfanyabiashara yeyote.

“Kama kuna mfanyabiashara yeyote humu ndani ambaye alinipa hata shilingi moja wakati wa kampeni anyoshe mkono,” Dk. Magufuli aliuliza. “ Nilikataa kupokea mchango wa mfanyabiashara yeyote kwa sababu nilitaka kufanya kazi tu,” aliongeza.

Mwanasheria Mkuu Awakana Wakuu Wa Mikoa Wanaositisha Likizo Za Watumishi
Magufuli Atoa Siku Saba Kwa Wafanyabiashara Waliokwepa Kodi