Rais John Magufuli ameweka wazi jinsi ambavyo hali ya rushwa ilikuwa imekithiri katika Serikali ya Awamu ya Nne na uwepo wa mtandao uliokuwa ukitumia njia za rushwa kupenyeza majina ili yateuliwe.

Akiongea jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa kuwaapisha Wakurugenzi Wapya wa Halmashauri mbalimbali nchini, Rais Magufuli alisema kuwa alikuwa makini na alitumia muda mrefu kuyahakiki kila jina moja la wateule hao baada ya kuubaini mtandao huo.

Magufuli na Wakurugenzi

Rais John Magufuli akitoa maagizo kwa Wakurugunzi wapya wa Halmashari

Alisema kuwa mtandao huo uliongozwa na vinara watatu kwenye Ofisi za Waziri Mkuu- Tawala za Mikoa na Serika za Mitaa (TAMISEMI), na kwamba tayari amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo ambayo hivi sasa iko chini yake awaondoe mara moja.

“Wapo waliotaka kupenyeza majina lakini yote nikayatupilia mbali. Mimi ndiye ninaewafahamu, nataka ninyi mkawatumikie vizuri wananchi, imani izae imani. Hamuhitaji kushangiliwa, wananchi watawashangilia vizuri mkitekeleza wajibu wenu,” Rais Magufuli aliwaambia wakurugenzi hao.

Aliwataka kuwa imara katika kusimamia haki na uwajibikaji na kuwawajibisha mara moja Makatibu Tarafa watakaoenda kinyume na muelekeo waliouchagua wa kuwatumikia wananchi.

Magufuli Aanika Rushwa za JK. Chadema yawekewa Ulinzi Kila Kona DOdoma
Video: Diamond ft P'Square - Kidogo