Mgombea urais kupitia CCM, Dk. John Magufuli ameeleza jinsi ambavyo serikali yake itakavyohakikisha wananchi wote wanafaidika na kazi wanazozifanya na kupewa ulinzi wa ajira zao hadi wafanyakazi wa NDANIi.

Dk. Magufuli ameyasema hayo jana wakati akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika Mkoani Mbeya ambao ulihudhuriwa na maefu ya wananchi.

“Wenye magari wote Tanzania, waanze kutoa mikataba kwa madereva, nataka hata kwa wafanyakazi wa ndani, wauza hotelini na ma-receiptionists…lazima wawe na mikataba. Tanzania hii uwe ukipata kazi unapata security ya kazi yako,” alisema.

Dk. Magufuli alieleza hayo masaa machache baada ya kufanyika kikao cha madereva na makondakta waliotangaza kusitisha mgomo wao baada ya kupewa nafasi ya kuonana na rais Jakaya Kikwete.

Mahakama Kuu Yatengua Hukumu Dhidi Ya Mbowe
Ivo Aungana Na Maftah Kulaani Kitendo Cha Nyosso