Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli ametoa onyo kwa wakuu wa shule zote za msingi na sekondari nchini ambao wamepokea mafungu ya serikali kwa ajili ya kugharamia elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne.

Akiongea jana wakati akiwa jijini Arusha baada ya wananchi kuziba njia wakitaka azungumze nao, Dk. Magufuli aliwataka wakuu wa shule kuhakikisha hawahujumu fedha zilizowafikia kwa ajili ya kugharamia elimu bure.

“Tutaendelea kupeleka fedha kwenye mashule yote. Nitoe wito kwa wakuu wa shule, wasicheze na hizo fedha,” alisema. “Wasicheze na hizo- fedha,” alisisitiza. “Hizo fedha ni kwa ajili ya wanafunzi watoto wa masikini wasome bure.”

Rais Magufuli alisisitiza kuwa serikali yake imejipanga na itaendelea kupambana na ufisadi na wizi wa mali za umma bila kujali wahusika.

Aliongeza kuwa serikali yake haitabagua vyama wala kabila bali itawatumikia wananchi wote bila kujali itikadi na lugha zao.

Javier Mascherano Ahukumiwa Kwenda Jela
Ushindi wa Tundu Lissu wapata baraka