Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amevitaka vyombo vya habari, Taasisi ya TCRA kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wazazi kukemea vikali mambo yanayochochea mmomonyoko wa maadili hasa kwa mabinti kwani tabia ya watoto wa kike kuonekana nusu uchi imekithiri.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye mkutano wa Jumuiya ya Wazazi mjini Dodoma, na kusema kwamba huwa anashangazwa kila anapowasha Television kutazama muziki, na kukutana na mabinti wakicheza utupu huku wanaume wakiwa na mavazi ya staha, na kusema kwamba ni aibu kubwa kwa wazazi kuangalia mambo hayo.

“Mimi ni shabiki mzuri wa muziki, kila ukifungulia mziki wanaocheza utupu ni wanawake wanaume hapana” Amesema Magufuli.

Hivyo amewataka jumuiya ya wazazi kukemea mambo hayo, kwani sio fundisho zuri kwa watoto.

Rais Magufuli ameitaka jumuiya hiyo na watu wote kusimamia maadili, huku akivinyooshea mkono vyombo husika vinavyopaswa kushughulika na masuala ya utamaduni wa Mtanzania.

“Ifike mahali sisi kama watanzania, bila kujali vyama vyetu, tulinde maadili yetu, amesema Rais Magufuli.

 

Muhimbili yatoa somo kwa watumishi wapya
JPM: Jumuiya tembeeni vifua mbele