Mgombea urais wa Jamuhuri ya Muungano kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli amesema endapo atapewa nafasi ya kuwa rais kwa muhula wa pili wananchi katika soko la mahakama ya ndizi hawatalipa ushuru.

kizungumza na wanachi wa eneo la Mburahati Jijini Dar es salaam mgombea huyo amesema anajua atashinda nafasi hiyo , hivyo atatumia mamalaka ya kiti hicho kufanya maamuzi na watalipia vitambulisho badala ya kulipa ushuru.

“Kwa sababu ninajua nitachaguliwa kwa mamlaka niliyonayo kama Rais, soko la Mahakama ya Ndizi litabaki chini ya wananchi wa eneo hilo, kuanzia leo wafanyabiashara wanaofanya hapo hakuna kulipa ushuru watalipia kitambulisho tu,” amesema Magufuli.

Aidha Magufuli amewashukuru na kuwasifu wanachi toka maeneo ya Dar es salaam kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za chama chake.

“Huu upendo mliounesha ni lazima tuulipe mara 100 kwa wananchi wa majimbo haya, kweli nimeguswa sijui niwafanyie nini, ndugu zangu niwalipe nini, sijui nianze na soko hili la Mahakama ya Ndizi, niambieni mnataka nifanye nini”

Dkt. Magufuli, kesho anatarajia kuendelea na kampeni katika jimbo la Kawe ambapo ataeleza sera zake pamoja na kuwanandi wagombea ubunge na madiwani kupitia CCM .

KMC kujiuliza kwa Coastal Union
Manara awafunda mashabiki uchwara