Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kimesema kuwa kitamfikisha mahakamani mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, Dk. John Magufuli kwa tuhuma za wizi na matumizi ya nembo ya chama hicho ya M4C, kinyume cha sheria.

Hayo yaliwekwa wazi na mwanasheria wa Chadema, John Mallya alipoongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam na kubainisha kuwa chama hicho kitafungua kesi hiyo chini ya hati ya dharura ili liweze kushughulikiwa haraka.

Mallya alieleza kuwa Chadema ilifuata taratibu zote za kusajili nembo hiyo katika ofisi za Msajili Wa Vyama vya Siasa pamoja na Wakala wa Biashara (BRELA) kwa ajili ya matumizi ya kibiashara kwa kuuza T-Shirt na kofia za chama hicho.

“Mgombea urais wa CCM amevunja sheria za nchi pamoja na mikataba ya makubaliano mbalimbali ya kimataifa na kikanda kwa kumama jukwaani na kuitumia nembo ya M4C ambayo imesajiliwa kisheria na Chadema,” alisema Mwanasheria wa Chadema.

Alitaja sheria nyingine zilizovunjwa kuwa ni pamoja na Sheria ya Alama za Biashara na Huduma (Trand and Service Mark Regulation) ya mwaka 2000. Pia, Dk. Magufuli anadaiwa kuvunja sheria ya kimataifa ya haki miliki (World Intellectual Property Organisation) ya mwaka 1979 ambayo Tanzania iliiridhia mwaka 1983.

Mwanasheria huyo wa Chadema alisisitiza kuwa ifikapo Jumatatu asubuhi watawasilisha mahakamani malalamiko yao chini ya hati ya dharura huku akiwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Bodi ya Wadhamini ya CCM pamoja na Timu yake ya kampeni.

Hivi karibuni, Mgombea urais huyo kupitia CCM, akiwa mkoani Kigoma aliwaeleza wananchi kuwa nembo inayotumiwa na Chadema ya M4C ambayo ina maanisha ‘Movement For Change’, haina maana hiyo bali ina maanisha ‘Magufuli For Change’.

Muda mfupi baada ya mgombea huyo kutoa kauli hiyo, nembo ya M4C ilianza kuonekana ikiwa kwenye mitandao ya kijamii ikiwa na jina la ‘Magufuli 4 Change’ huku ikidaiwa kuwa chama hicho kina nia ya kuandaa T-Shirt zenye nembo hiyo.

Kwa mujibu wa Chadema, Nembo hiyo iliasisiwa mwaka 2006 ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha kampeni ya mabadiliko na ilifuata taratibu zote za kisheria katika kuandisha..

 

NCCR- Mageuzi Waeleza Njama Za Kumuua James Mbatia
Eva Carneiro Amuweka Mtegoni Mourinho