Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Magufuli, jana aliwaongoza wanachama wa chama hicho kuupokea mwili wa Dtk. Abdallah Kigoda aliyepoteza maisha nchini India, ambapo ameeleza kuwa alimpa ushauri katika kipindi kifupi kabla Mungu hajamchukua.

Akiongea na waandishi wa habari, Magufuli alieleza kuwa Marehemu Kigoda alimshauri masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na jinsi ya kuwasaidia wawekezaji na wafanyabiashara wazalendo.

“Alinipa ushauri mwingi tu wa masuala ya namna ya kuwawezesha wafanyabiashara wazalendo na watanzania, namna ya kujenga uchumi. Na akawa amenitumia e-mail, na hicho ndicho kilikuwa cha mwisho ambacho nilikipata kutoka kwa mheshimiwa Dkt. Kigoda,” alisema.

Dkt. Magufuli alimuelezea alimuelezea Dkt. Kigoda kama mtu aliyekuwa anaipenda kazi yake pamoja na kuwa na upendo hasusan kwa wananchi wa jimbo la Handeni aliokuwa akiwawakilisha bungeni.

 

 

Rais Kikwete Aonya Wanaobaki Vituoni Kulinda Kura, Mbowe Aja Na Yake
Ronaldo Hakamatiki Kwa Sasa