Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli ameendelea kutangaza vita dhidi ya ufisadi akijifananisha na maji ya moto dhidi ya mafisadi.

Akiongea na waanchi mkoani Mtwara, Magufuli aliwafananisha mafisadi na ‘kunguni’ waliojificha kwenye kitanda ambao dawa yao ni kuwamwagia maji ya moto.

“Mimi ni maji ya moto wa mafisadi, nipeni urais muone nitakavyowaunguza,”alisema Dk. Magufuli.

Katika hatua nyingine, Dk. Magufuli alisisitiza kuwa atahakikisha anamaliza tatizo la maji katika mkoa huo na kwamba waziri wa maji atakayemchagua hatakaa Dar es Salaam na kusherehekea wiki ya maji wakati wananchi hawana maji.

PFA Wamkingia Kifua Saido Berahino
Marotta: Thamani Ya Pogba Ilikua Euro Milion 100