Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli ameeleza sababu za kutoboresha maslahi ya wafanyakazi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ambacho amekuwa rais.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni wilayani Korogwe mkoani Tanga Magufuli amesema kuwa hakupandisha mishahara kwa kuwa alikuwa akiboreshakwanza uchumi wa nchi, kuondoa wafanyakazi hewa na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji kodi ili kuongeza mapato ya nchi.

“Katika kipindi cha miaka mitano itakuwa kazi pia ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi wa Tanzania, unaanza uchumi kwanza ndipo utapandisha mishahara, huwezi kupandisha mishahara wakati huna hela ya  kupandisha mishahara,”amesema Magufuli.

Magufuli amesema endapo atashinda nafasi hiyo ataboresha maslahi ya wafanyakazi na kuwataka wananchi kuchagua chama kitakacholeta maendeleo na si mambo mengine.

“Wakati wa Uchaguzi ndiyo wakati wa kuamua kama mnataka maendeleo au mnataka braa braa, mnataka amani au mnataka kuandamana, mnataka upendo au mnataka vurugu, siku hiyo ya tarehe 28 ni siku ya kuamua”.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 21, 2020
NEC yaifuta adhabu ya Mbatia