Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amewataka Watanzania kuendelea kumuomba Mungu aliepushe Taifa dhidi ya Ugonjwa wa Corona na kusisitiza kuwa hatatangaza ‘Lockdown.’

Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akiongoza waombolezaji kuuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 19, 2021.

“Tusitishane na kuogopeshana Mungu yupo, Mungu ndiyo muweza wa yote. Tuendelee kusimama na Mungu, tulishiinda Corona mwaka jana. Naomba Tusimame na Mungu,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ametoa pole kwa watanzania wote kwa kuondokewa na Maalim Seif pamoja na Balozi Kijazi, ambapo amesema kuwa alimtuma Makamu wa Rais na Dkt. Bashiru wamuwakilishe kwenye mazishi ya Maalim Seif.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amesitikitishwa na watu wanaozusha taarifa za uongo kwamba Waziri wa Fedha, Dkt. Philip Mpango amefariki dunia huku akisoma SMS aliyotumiwa na Dkt. Mpango kuhusu hali anayoendelea nayo.

Marekani kurejea katika mkataba wa nyuklia
PICHA: Clube Deportivo 1° de Agosto waanza safari ya Bongo