Mgombea nafasi ya urais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania   kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ,Dokta John Magufuli amewaomba wafuasi wa chama hicho na wananchi kwa ujumla kutobaguana kwa namna yoyote.

Akihutubia mkutano wa kampeni za CCM katika eneo la Ifunda wilayani Makambako  , Magufuli amewaomba wananchi kuwa pamoja hata baada ya uchaguzi kupita.

“Nawaomba tuendelee kujenga umoja tusibaguane kwasababu ya Vyama, Dini wala Ukabila, sisi ni Taifa moja, Mwl Nyerere katuacha tukiwa wamoja, naomba Uchaguzi usitugawe, nawaomba Wana- CCM, CHADEMA, ACT, CUF na Vyama vingine vyote tushikamane” amesema Magufuli.

Mgombea huyo amewashukuru wananchi wa eneo kwa kujitokeza kwa wingi kwenye kampeni za chama hicho na kuwataka wanachama wa vyama vingine mkoani Njombe na Iringa kuchagua CCM.

Bofya hapa……

Wanne mbaroni, tuhuma za mauaji ya kiongozi UVCCM Iringa
Mikopo inatuchelewesha- Rais Shein

Comments

comments