Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ametoa wito kwa wananchi kuacha kudharau dawa za kienyeji na matumizi yake katika matibabu ya magonjwa mbalimbali kwani Mugu ameumba mimea isaidie binadamu.
Amebainisha hayo leo Juni 11, alipokuwa anazindua ofisi za Wakala wa Bararaba Mijini na Vijijini (TARURA), Mji mkuu wa Srikali jijini Dodoma.
“Tusidharau dawa za kienyeji, tusidharau hata kidogo, uchawi tu ndiyo mbaya lakini miti yote iliumbwa na Mungu kwaajili ya kutusaidia sisi” Amesema Magufuli
Ametoa agizo kwa wizara ya afya kuongeza bajeti kwenye kitengo cha tiba asili na kuamini dawa hizo kama zilivyo saidia kwenye mapambano dhidi ya Corona.
“nimeshatoa maelekezo kwenye wizara ya afya, kile kitengo cha dawa asili kiendelezwe kwa nguvu zote na bajeti yake iongezwe, ili watu wanapotengeneza madawa tusiwadharau” Amesisitiza JPM
Ametolea mfano hata kwa nchi ambazo zimeendelea kiteknolojia kama china, Amerika na Canada kuna maduka ya dawa asili ambazo wametengeneza na wanazitumia.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kwani corona imepungua sana lakini haijaisha hivyo mapambano yanaendelea bila kusahau kuendelea kumuomba Mungu.