Beki Harry Maguire amekiri wanapaswa kukaa na klabu yake ya Mandhester United kuzungumza kama ataendelea kucheza mara moja kwa mwezi.

Mlinzi huyo wa kati wa kimataifa wa England amepata mashaka na kukosa nafasi ya kutosha ya kucheza kwenye kikosi cha Mashetani hao Wekundu kiasi cha kumfanya avuliwe kitambaa cha unahodha wa timu hiyo.

Maguire, mwenye emri wa miaka 30 alihusishwa kujiunga na klabu ya West Ham wakati wa majira ya kiangazi lakini mpango huo haukukamilika na kusalia kwenye kikosi cha Manchester United akidhamiria kumshawishi kocha wa timu hiyo, Erik ten Hag kumpatia nafasi ya kucheza.

Huku fainali za Mataifa ya Ulaya ‘EURO 2024’ zikikaribia, Maguire amesema kukosa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha Manchester United kunaweza kuhatarisha nafasi ya kuitwa kwenye tinu ya taifa ya England.

Kocha Mkuu wa England, Gareth Southgate amekuwa shabiki mkubwa wa beki huyo wa kati pamoja na kupita kwenye wakati mgumu katika maisha yake ya soka ambapo beki huyo amedhamiria kuboresha kiwango chake.

Fei Toto: Waambieni kitaeleweka Oktoba 25
Mashujaa FC: Simba SC wameponyoka mtegoni