Huduma za tiba mbadala nchini zimeendelea kupata wateja wengi na kuwapa utajiri mkubwa baadhi ya watu wanaojitangaza kwenye vyombo vya habari kutoa huduma hizo.

Moja kati ya sababu kubwa zinazowafanya watu hao kuaminika na kupata wateja wengi ni namna wanavyoweza kutumia kifaa cha kisasa cha Quantum Magnetic Resonance Analyser kilichotengenezwa nchini China na Korea Kusini ambacho watengenezaji wake hudai kina uwezo wa kufanya uchunguzi kwa nguvu ya sumaku na kupata taarifa za mwili mzima ndani ya dakika moja tu bila kumtoboa mgonjwa.

Mashine ya Quantum Magnetic Resonance Analyser inavyochukua vipimo vya mgonjwa vya mwili mzima

Mashine ya Quantum Magnetic Resonance Analyser inavyochukua vipimo vya mgonjwa vya mwili mzima

Mwandishi wa gazeti la The Citizen aliamua kufanya uchunguzi (investigative journalism) ili kubaini ukweli au ulaghai unaofanywa na watoa huduma hizo za tiba mbadala kwenye kliniki zao na kujipatia utajiri mkubwa kutokana na kujihusisha na afya za binadamu.

Katika moja kati ya njia alizotumia mwandishi huyo, alimtuma Allan Sembaza ambaye ni baba wa watoto wawili aliyefika katika moja ya kliniki maarufu jijini Dar es Salaam kupata huduma. Sembaza alieleza kuwa ameshindwa kupata mtoto hivyo angependa kujua tatizo lake na kupata matibabu.

Sembaza aliambiwa atoe kiasi cha shilingi 40,000 ili aweze kuonana na daktari na kupata vipimo. Sembaza ambaye ni mkazi wa jiji la Dar es Salaam alimueleza mwandishi huyo kuwa alionana na daktari aliyejitambulisha kwa jina moja la ‘David’, ambaye alimueleza kuwa kipimo cha Quantum Magnetic Resonance Analyser kimeonesha kuwa hana uwezo wa kupata mtoto.

Daktari huyo alimueleza kuwa anapaswa kutumia dawa za tiba mbadala kwa muda wa miezi mitatu ambazo alitakiwa alipie shilingi 320,000. Alimhakikishia kuwa baada ya kutumia dawa hizo tatizo lake litakuwa limekoma na ataweza kupata mtoto.

Mbali na ushahidi huo, Mwandishi huyo alifanya mahojiano na wagonjwa mbalimbali waliowahi kupata huduma ya tiba mbadala kwenye kliniki husika na kubaini kuwepo na udanganyifu unaotumia mashine hizo za vipimo kurubuni na kupata fedha.

Jerome Sungura, mkazi wa jiji la Dar es Salaam alimwambia mwandishi huyo kuwa walifika katika moja ya kliniki akiwa na mchumba wake aliyekuwa anasumbuliwa na tumbo. Alishawishiwa na daktari kufanya vipimo kwa kutumia mashine ya Quantum Magnetic Resonance Analyser ambayo aliambiwa inatumika kwa siri kwa kuwa serikali haijatoa kibali cha kuiingiza nchini.

Hata hivyo, baada ya kufanya vipimo kwa muda wa dakika moja tu, aliambiwa mchumba wake ana tatizo la upungufu wa vitamini E na kwamba homoni zake hazina usawa (hormonal imbalance). Hali hiyo ilimfanya aamini kuwa vipimo hivyo vilikuwa ‘magumashi tu’.

Marufuku uvaaji Vimini, Mlegezo
Kafulila Adai NEC Inahujumu Kesi Yake Ya Uchaguzi, NEC Yamruka