Askari wa Jamii (VGS) Jumuiya ya hifadhi ya Wanyamapori Enduiment (EWMA), Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha wamekamata magunia matano ya bangi katika Kitongoji cha Engutukoit Kijiji cha Losinoni Kata Oldonyouwasi Wilayani Arumeru mpakani na Kijijini cha Ngereyan Wilaya ya  Longido.

Akizungumza na Dar24 Media Meneja wa jumuiya hiyo Peter Millanga amesema usiku wa kuamkia Mei 27 askari walifankiwa kukamata pikipiki ikiwa  na gunia tano za bangi iliyotelekezwa  na dereva baada ya kuona amesimamishwa na maaskari hao  eneo la Engutukoit ukanda wa Ngereyan ambapo  zilikuwa zinasafirishwa kwa njia za panya kuelekea Kenya.

“Mhusika hakuweza kukamatwa kwani alipozidiwa alitelekeza pikipiki na mzigo wake na kufanikiwa kukimbia,” amesema  Millanga.

Aidha Millanga amesema kuwa  walipokea taarifa kutoka kwa msiri wao (informer) na kuamua kuifanyia kazi taarifa hiyo na ndipo wakafanikisha kukamata magunia hayo.

Hata hivyo Millanga na timu yake waameshaliwasilisha swala hilo la kwa  Mkuu wa Jeshi la Polisi wilaya na kupeleka vithibitisho hivo ili jitihada za kumtafauta mtuhumiwa ziweze kuendelea.

Serikali yaahidi kusimamia bei za mazao
Makapu atema nyongo Young Africans