Mshambuliaji wa Geita Gold, Elias Maguri ameanza vyema Ligi Kuu Bara msimu huu akiwa mfungaji wa kwanza akifunga bao dakika ya tano tu wakati wakiizamisha Ihefu FC, jijini Mbeya na bao hilo limemfanya nyota huyo kutamba akisema anatamani kuvuka rekodi ya mabao aliyomaliza nayo katika ligi iliyopita.

Msimu ulioisha Maguri alijiunga na timu hiyo katika dirisha dogo na kuifungia mabao saba, lakini amesema safari anataka kuivuka rekodi hiyo na anaona atakuwa na nafasi kubwa ya kufanya vyema akipigania timnu yake na kuvuka lengo hilo.

“Nashukuru Mungu nimeanza kwa kucheka na nyavu. Hilo ni tamanio la kila Mshambuliaji, jambo kubwa kwa kushirikiana na wenzangu ni kuisaidia timu kupata matokeo ya ushindi kwani ninavyouona msimu huu utakuwa mgumu kuliko uliopita,” amesema.

“Msimu ulioisha niliingia Geita Gold katika dirisha dogo baada ya kukaa nje miezi kadha bila timu. Ndio maana natamani ligi ya msimu huu nifunge mabao mengi zaidi ya yale saba, kikubwa ni ushirikiano wa timu nzima na tunajenga kwa pamoja.

Mchezaji huyo, amesema pamoja na kutamani kufunga mabao mengi jambo la msingi kwake ni kupigania malengo ya timu ya kuhakikisha wanamaliza nafasi za juu.

Wachezaji wote tupo kwa ajili ya Geita, kabla ya malengo binafsi lazima tutangulize  yaliyotukuatanisha hapa.”

Mbeya wahimizwa ibada kunusuru ndoa kuvunjika
Sisi ni Binadamu sio Nyani, tutambuane