Bingwa mtetezi wa michuano ya Australian Open, upande wa wanaume Novak Djokovic amepangiwa kuanza kutetea ubingwa wake kwa mwaka 2016, kwa kupambana na mshiriki kutoka Korea Kusini, Chung Hyeon anayeshika namba 51 kwa ubora duniani.

Ratiba ya michuano hiyo kwa mwaka 2016 iliyotolewa hii leo, imeonyesha gwiji mwingine katika mchezo wa Tennis, upande wa wanaume Andy Murray ambaye alishindwa kufurukuta katika mchezo wa hatua ya fainali mwaka 2015 kwa kufungwa na Djokovic, amepangiwa kuanza na Alexander Zverev kutoka nchini Urusi.

Kigogo mwingine ambaye anautikisa ulimwengu katika mchezo wa Tennis Roger Federer, naye amepangiowa kuanza na mshiriki kutoka nchini Georgia, Nikoloz Basilashvili ambaye anashika nafasi ya 117 kwa ubora duniani.

Bingwa wa michuano hiyo kwa mwaka 2014, Stan Wawrinka, atapambana na mshiriki kutoka nchini Urusi, Dmitry Tursunov ambaye kwa sasa anakamata nafasi ya 265 kwa ubora duniani.

Bingwa wa mwaka 2009, Rafa Nadal amabye yupo katika nafasi ya nne kwa ubora duniani, ataanza kuusaka ufalme wa Australian Open mwaka 2016 kwa kuonyeshana kazi na mspaniola mwezake, Fernando Verdasco.

Man city Wafanya Usajili Wa Kushangaza
Heather Watson Atupwa Nje Hobart