Mrembo maarufu wa Kenya, Huddah Monroe ameweka wazi kuwa anavutiwa na muonekano wa Jux na kumfungulia milango ya kuwa naye kwenye mahusiano ya mapenzi.

Huddah ‘The Boss Chick’ amefunguka kwenye Nirvana cha EATV akieleza kuwa amekuwa akivutiwa na muonekano wa Jux pamoja na jinsi anavyopangilia mavazi yake na yanavyomkaa vyema.

“Nafikiri ni mwanaume ambaye naweza kuwa naye kwenye mahusiano… Yupo ‘single? Hata mimi nitapatikana…” Huddah alifunguka akijibu swali kama anaweza kuwa mahbuba wa Jux.

Katika hatua nyingine, mrembo huyo amemshauri Jux kuwashirikisha wasanii wa kimataifa ili aweze kuwa msanii mkubwa zaidi kwani muonekano wake na kazi yake vinamuongezea sifa za kuwa msanii mkubwa wa kimataifa.

 

Aidha, Huddah amekiri kwamba amewahi kumcheki Jux kupitia Instagram na kumwambia jinsi gani anapenda muonekano wake wa mavazi.

Ebitoke afunguka chanzo kikuu cha kuachana na Ben Pol
Beka Flavour 'aikataa' Yamoto Band