Mahabusu ambaye alikuwa na kesi ya mauaji, Musa Haji Mchana, amepigwa na radi Oktoba 13 na kupoteza maisha kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ukanda wa Pwani.

Aidha wafungwa wanne ambao ni Richard Simau, Issa Haji, Hashim Rashid na Ismail Mtupa wamejeruhiwa na radi hiyo na hivi sasa wako hospitali wakiendelea na matibabu .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga amesema gereza lililopata kadhia hiyo ni gereza la Wilaya linaloitwa Mng’aro lililoko Kibiti.

Kamanda Lyanga ameongeza kuwa hakuna wafungwa wala mahabusu waliotoroka baada ya kupigwa na radi hiyo na ulinzi umeimarishwa zaidi.

G20 kujadili uchumi wa dunia
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 14, 2020

Comments

comments