Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetangaza kuanza kusikiliza kesi inayomkabili mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kuanzia August 28, 2016.

Tundu Lissu amefikishwa Mahakamani akituhumiwa kwa kosa la kutoa lugha ya uchochezi kwa Rais John Pombe magufuli aliyoitoa June 28, 2016.

Akitoka mahakamani hapo, Tundu Lissu amesema kuwa wamesajiliwa na wanahaki ya kufanya mikutano.

“Hizi kauli kwamba ukafanyie mahali ulipochaguliwa ni zamtu anayefikiria hasomi sheria, anafikiria kila linalokuja kichwani mwake anaona hili ndiyo sheria, na huo ndiyo udikteta tunaoukataa na tutaendelea kukukataa” – Tundu Lissu

Katika hatua nyingine Mahakama ya hakimu mkazi Arusha imemwachia huru Mbunge wa Arumeru  Mashariki, Joshua Nasari na Madiwani 29 waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uharibifu wa mali baada ya upande wa mashitaka kuondoa shauri hilo.

 

Mohamed Dewji 'MO' Akabidhi Mzigo Wa Usajili Simba SC
Young Africans Waitwa Kwenye Mkutano Mkuu