Jaji Edwin Kakolaki wa Mahakama Kuu amesema kwa sasa HAKUNA suala la dharura la mahakama hiyo kusitisha mchakato wa uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF).
Wanasheria watatu wanaomtetea, Ally Salehe aliyeenguliwa kwenye mchujo wa awali kuwania urais wa TFF waliwasilisha ombi la mchakato wa uchaguzi huo utakaofanyika Agosti 7 mjini Tanga kusimamishwa hadi kesi yao ya msingi itakaposikilizwa.
Nje ya mahakama, mmoja wa wanasheria wanaomtetea Ally Salehe, Stephen Mosha amesema shauri dogo la zuio la uchaguzi huo litatolewa hukumu Julai 9 na kesi ya msingi pia itasikilizwa siku hiyo.