Mahakama nchini Kenya imewaruhusu Wasichana wa kiislam wanaosoma shule nchini humo   kuvaa hijab kama sehemu ya sare zao za shule

Uamuzi huo umetolewa  na majaji watatu mara baada ya kanisa la kimethodist kupinga muongozo kutoka kwa mamlaka za nchi hiyo za kuwaruhusu wasichana wa shule wa kiislamu kuvaa hijab au vilemba katika shule yake.

Wanafunzi wa kiislam wanaosoma katika shule hiyo ya sekondari ya St Paul Kiwanjani School kaunti ya Isiolo walipigwa marufuku kuvaa hijab na suluari nyeupe pamoja na sare ya shule.

Kanisa hilo lilidai kuwa uamuzi wa kuwaruhusu wanafunzi wasichana wa kiislamu kuvaa mavazi tofauti umesababisha uhasama miongoni mwa wanafunzi.

Lakini majaji katika mahakama ya rufaa wamesema kuwa ni jukumu la wanaotoa elimu kukubali maadili na kanuni za utu na za matabaka mbali mbali ya watu bila ubaguzi.

Mourinho Azidi Kuhaha Kuelekea Mchezo wa Derby,Mchezo Kati ya Manchester United na Manchester City
Waziri wa Maji Gerson Lwenge Awasimamisha Kazi Mameneja 9 Kwa Tuhuma za Wizi Wa Kimtandao za Maji