Mahakama nchini Uganda imeamuru Polisi ambao wamemuweka kizuizini Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine na kutomruhusu kutoka kwake tangu alipopiga kura Januari 14, watoke nyumbani hapo na wamuache Bobi awe huru.
Mahakama imesema ni kinyume cha sheria na uvunjifu wa haki kuendelea kumzuia Bobi na kusema kama ana makosa afikishwe Polisi au apelekwe Mahakamani.
Polisi nchini humo wamemuweka kizuizini Bobi wakidai wanazo taarifa kuwa akiwa huru anapanga kuwachochea Vijana kushiriki katika ghasia.
Bobi ambaye ni mpinzani mkubwa wa Rais Museveni alishika nafasi ya pili kwenye Uchaguzi uliomuweka tena Madarakani Museveni.