Hakimu katika Mahakama Kuu ya Shanzu, Yusuf Abdallah, ameamuru Polisi kuendelea kuwazuilia Muhubiri Paul Mackenzie, mkewe Rhoda Mumbua na washukiwa wengine 16 kwa muda wa siku 23 zaidi.
Abdallah ametoa amri hiyo kutokana na upande wa mashitaka kudai kuwa bado haujakamilisha upelelezi na kwamba shughuli ya kufukua miili pia inaendelea hivyo washukiwa waendelee kukaa ndani wakihofu huenda wakaharibu ushahidi.
Awali upande wa mashtaka ulitaka washukiwa hao kuendelea kuzuiliwa kwa muda wa miezi mitatu zaidi, lakini uamuzi wa Mahakama umetoa muda huo ili kutoa nafasi kwa wapelelezi kuendelea na shauri lao kwa muda uliopangwa.
Katika hatua nyingine, Msajili wa mashirika ya kijamii ametoa muda wa siku 30 kwa Kanisa la Mhubiri huyo wa Kanisa la Good News na lile la la Mhubiri Ezekiel Odero la New Life Prayer Center, kueleza kwanini makanisa hayo yasifungwe baada ya kukosa kuzingatia sheria za usajili wa mashirika ya kijamii nchini.