Kupitia sakata lililozuka mitandaoni kuhusu Nabii Tito ambaye ameonekana akifanya mahubiri ya kichochezi, serikali iliamuru kumchukulia hatua za kisheria kutokana na kufanya mahubiri hayo kinyume na maadili ya dini.
Kupitia kesi hiyo inayomkabili, Mahakama ya Wilaya ya Dodoma imemuamuru Mkuu wa Gereza la Isanga kumpeleka hospitali kuu ya magonjwa ya akili, Mirembe, mkazi wa kijiji cha Nong’ona Tito Onesmo Machibya maarufu kama (Nabii Tito), ili kuchunguzwa kama ana ugonjwa wa akili au la.
Hakimu mfawidhi wa Mahakama hiyo James Karayemaha amesema anahitaji majibu hayo mnamo Marchi 5 mwaka 2018 siku ambayo mtuhumiwa huyo atafikishwa Mahakamani ikiwa ni baada ya agizo la mtuhumiwa huyo kupimwa akili kutotekelezwa hapo awali.
-
Wolper: Tanzania jina la nchi yetu naona si tamu tena na limeanza kuwa chungu
-
Chadema wataka Polepole ahojiwe
Nabii Tito Machibya alifikishwa Mahakamani hapo akituhumiwa kufanya uchochezi wa kidini kupitia mafundisho anayo yatoa na amekuwa akiieleza Mahakama kuwa amekuwa akifanya hivyo kwa sababu ana matatizo ya akili na kutoa vithibitisho toka hospitali ya Taifa Muhimbili.