Mahakama kuu Nchini Kenya imeamuru kuwashwa kwa vituo vitatu vya runinga binafsi na vya Serikali na kuiagiza Serikali kutoingilia utendaji kazi wa vituo hivyo hadi kesi hiyo itaposikilizwa kikamilifu.

Kesi hiyo imekuja kufuatia sakata la kuapishwa kwa kiongozi wa muungano wa vyama vya upinzani (NASA) nchini Kenya, Rais wa watu Raila Odinga.

Ambapo Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta aliviamuru na kuvizuia vyombo vya habari televisheni na Radio kurusha tukio hilo hewani kwani ni tukio lililotendeka kinyuma na Sheria ya nchi hiyo.

Hivyo kufuatia agizo hilo vyombo vyote vya habari nchini humo vilizimwa kupisha kufanyika kwa tukio hilo kama ilivyoagizwa na Rasi wao Uhuru Kenyetta.

Vituo vilivyozimwa ni pamoja na KTN, NTV na Citizen TV.

 

Video: CUF, Chadema watunishiana misuli Kinondoni
Majibu ya Serikali matumzi ya sindano za kuongeza maumbile