Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam imeagiza kukamatwa kwa washtakiwa, Freeman Mbowe na Esther Matiko kwa kutofika mahakamani kusikiliza kesi yao na viongozi wengine wa CHADEMA hii leo kinyume na masharti ya dhamana.

Kesi inayowakabili viongozi wakuu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA imeendelea kusogezwa mbele mara baada ya aliyekuwa wakili wa anayemtetea Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Petter Msigwa Wakili Jamhuri Johnson kutangaza kujiondoa.

Aidha, uamuzi wa kujiondoa kwa wakili wa Msigwa ambaye ni miongoni mwa washtakiwa wa makosa mbalimbali kwenye kesi hiyo umetokana na kile alichokidai kuwa haridhishwi na mwenendo wa kesi hiyo akisema kuwa katika miaka 20 ya uwakili wake, hakuwahi kuona kesi inaendeshwa kwa namna hiyo.

Awali, washtakiwa hao walisomewa maelezo ya awali lakini waligoma kujibu lolote kwa madai ya kuwa kutokuwepo kwa wakili wao. Kwa upande wake mdhamini wa mshtakiwa wa kwanza, Freeman Mbowe, ameieleza mahakama kuwa bado yuko nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Hata hivyo, viongonzi wakuu wa Chama hicho wanakabiliwa na makosa mbalimbali ikiwemo kosa la kuhamasisha uchochezi na kusababisha kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji Taifa (NIT), AkwIlina Akwilini

 

Watu 12 wafariki dunia shambulizi la Califonia nchini Marekani
Humoud arudisha mashambulizi KMC