Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara, imemtaka Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi afike mahakani hapo kutoa utetezi wake, kwanini mahakama hiyo isimhukumu kufungwa jela kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya kuwalipa shilingi bilioni 1.2 watu watatu.

Mengi aliamriwa kuwalipwa kiasi hicho cha fedha wafanyabiashara waliotajwa kwa jina la Muganyizi Lutagwaba, Eric Mshauri na Charles Mgweo. Malipo hayo yalitokana na uamuzi wa Mahakama kuhusu mgogoro wa hisa uliokuwepo   katika Kampuni ya Douglas Lake Minerals Ltd ambayo kwa sasa inaitwa Handeni Gold Inc. Hukumu hiyo awali ilitolewa Januari 28 mwaka huu na Jaji Agathon Nchimbi.

Walalamikaji wamewasilisha maombi ya mahakamani hapo wakiitaka mahakama hiyo kuchukua hatua dhidi ya Mengi ikiwa ni sehemu ya hatua ya kukazia hukumu iliyotolewa awali ya kuwalipa watu hao.

Hati ya kiapo ya wafanyabiashara hayo imeoenesha kuwa mmoja wa watu hao anaidai kulipwa fidia ya $428,750, mwingine $100,000 na mwingine $70,000.

 

Pazia La Ligi Kuu Tanzania Bara 2016/17 Kufunguliwa Kesho
TFF Yamruhusu Hassan Kessy Kuitumikia Yanga, Endapo Atalipa Mamilioni