Siku chache baada ya kutoka gerezani na kuanza kutumikia kifungo cha nje kwa kosa la kuua bila kukusudia , Mahakama ya Rufaa (Supreme Court of Appeal) nchini humo imemtia hatiani Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius.

Mahakama hiyo imemtia hatiani mwanariadha huyo kwa kosa la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa kumfyatulia risasi.

Jaji wa mahakama hiyo, Eric Leach alieleza kuwa Oscar alifyatua risasi kuelekea bafuni nyumbani kwake ili hari akifahamu kuwa kuna mtu ndani na kwamba angeweza kumuua. Alisema kuwa utetezi kuhusu nani ambaye alikuwa bafuni humo hauna tija kwa sababu Oscar alipaswa kujiridhisha mwenyewe kabla ya kuchukua uamuzi wa kufyatua risasi nne zilizompata mpenzi wake.

Mwanariadha huyo hivi sasa anatakiwa kurudi mahakamani kusomewa kifungo chake kwa mara nyingine. Kiwango cha chini cha kifungo cha kosa la mauaji nchini humo ni miaka 15 jela.

Mwanamuziki mkongwe Kasongo Mpinda aaga dunia
Watu 14 Wauwawa Kwa Risasi Marekani