Mahakama ya rufaa nchini Mareni imeendelea kuonyesha msimamo dhidi ya Rais wa Taifa hilo, Dolnad Trump baada ya kutupilia mbali ombi la kutaka kurejeshwa amri yake ya kupiga marufuku wahamiaji na wageni kutoka nchi saba kuingia Marekani.

Mahakama hiyo imechukua uamuzi huo mara tu baada ya ombi hilo lililowasilishwa mahakamani kutoka kwa idara ya haki nchini humo likiitaka mahakama kurejesha amri ya Trump.

Serikali ilikuwa imeitaka mahakama kurejesha amri hiyo baada ya uamuzi wa jaji kwenye mahakama ya Seatttle wa kupiga marufuku amri hiyo.

Baada ya mahakama kutupilia mbali rufaa hiyo, Trump alikashifu uamuzi huo wa jaji akisema kuwa unaiweka Marekani kwenye hatari ya kushambuliwa na magaidi.

Mashirika makubwa ya usafiri wa ndege, yangali bado yanawakubalia raia kutoka mataifa hayo husika, kuabiri ndege na kuingia Marekani.

Katika hatua nyingine, Trump ametetea uhusiano wake na Rais Vladimir Putin, katika mahojiano ya Runinga, huku akikataa kupinga madai ya mtangazaji kuwa Rais huyo wa Urusi ni muuaji.

Katika mahojiano ambayo yatarushwa na runinga ya Fox News leo Jumapili, Trump ameashiria kuwa Marekani isijifanye kutokuwa na hatia, kwani pia ina wauaji wengi.

Amesema itakuwa jambo bora zaidi ikiwa Urusi itasaidia Marekani kupambana na wanamgambo wa kundi la Islamic State.

Kinara wa madawa ya kulevya anaswa Mexico
Trump apinga amri ya mahakama, akata rufaa